Monday, December 12, 2011

BAADA YA MASOMO SOCIALIZATION INAENDELEA

Hivi ndivyo ilivyokua kwa wanafunzi wa tumaini university turdaco pale walipokutana kutoka campus zote nne na kula bata kiulainii na kusahau maisha na kero za chuo ndani ya masaa kadhaaaaa

Tuesday, December 6, 2011

BUNGE LAUNDA KAMATI YA UCHUNGUZIBunge la serikali ya wanafunzi ya chuo kikuu cha tumaini dar es salaam TURSODACO limeunda kamati ya uchunguzi kuchunguza ubadhilifu wa pesa za wanafuunzi katika wizara ya michezo na jamii.

Wabunge  walikutana jana kujadili shtuma zilizoletwa na serikali ya wanafunzi kufuatia matumizi mabovu ya pesa za wanafunzi zilizo tolewa kwa lengo la kufanyika kwa sherehe za kuwakalibisaha wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2011.

Wizara husika iliomba zaidi ya milioni tanao katika serikali ya wanfunzi kwa lengo la kukamilisha  na kufanikisha kwa sherehe hizo.hivyo bunge la wanafuzi lili lidhia bajeti hiyo kutokana na mahitaji yaliyo bainishwa katika kufanikisha kwa sherehe hiyo na waziri husika,kwani alidai kungekuwepo na ulinzi kutoka katika makampuni yanayojishirikisha na ulinzi,ungejengwa uzio kwa lengo la kuzuia wanafunzi kutoingia baharini usiku,ingejengwa steji,na wanafunzi wangepewa vinywaji kama soda na maji.

Kwa mujibu wa wanafuzi waliohudhulia sherehe hiyo wanadai hivyo vitu vyote vilivyoaidiwa havikuwepo,jambo lililosababisha wanafunzi kutaka kumpiga waziri husika kwani walio9na wamedanganywa,nae makamu wa Raisi wa Serikali ya wanafunzi mbwayu amekili kwamba ahadi alizotoa waziri wake hazikutimia,hivyo serikali ilingia wasiwasi wa utendaji wa waziri huyo hivyo walimuandikia barua kutaka apumzike ili uchunguzi ufanyike.

Waziri husika sulleman adamu aliandika barua kwa serikali ya wanafunzi kuomba kujiuzulu ili apishe uchunguzi ufanyike juu yake,hivyo kamati ya jumla ya watu wa tano ikiongozwa na mwenyekiti nyalusi kamati itaanza kazi rasmi wiki hii na kutoa report siku litapofanyika college baraza.